Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya amesema Halmashauri hiyo inaweka mikakati ya kuchangia ukamilishaji wa miradi mbalimbali yakiwemo maboma katika Sekta ya Afya na Elimu.
Mwl.Makwinya amesema hayo alipotembelea Zahanati ya Kandashe,Kata ya Leguruki ambapo mbali na huduma kuanza kutolewa Zahanati hiyo haina Nyumba ya mtumishi.
Aidha, Mwl.Makwinya ameuekeza Uongozi wa Kata hiyo kuharakisha ujenzi wa Nyumba ya mtumishi kufikia hatua ya lenta, ambayo kwa sasa bado ipo hatua ya Msingi ili Halmashauri kuona namna ya kuchangia "uhitaji ni mkubwa kila Kata ina miradi inayohitaji mchango wa Halmashauri, tutapitia miradi yote na kuona namna ya kusaidia " amesema Mwl.Makwinya
Nae Diwani wa Kata ya Leguruki Mhe.Nathanael Sikawa ameomba Halmashauri kuunga Mkono ujenzi wa nyumba ya Mtumishi katika Zahanati hiyo pamoja na kusaidia ukamilisha wa ujenzi wa shimo la kuhifadhia Kondo la nyuma .
Kata ya Leguruki ni Miongoni mwa Kata saba(7) ambazo Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa