• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Zaidi ya Millioni 997 Umetolewa Kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenyeulemavu.

Imewekwa: September 2nd, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wilayani Arumeru kwa kipindi cha miaka 5 kupitia mapato yake ya ndani  imetoa  zaidi ya Shilingi milioni 997,300,300  kwaajili ya mikopo kwa vikundi 374 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema fedha hizo zinakamilisha kiasi cha Mkopo uliotolewa kwa kipindi cha miaka mitano (kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2019/2020) kuwa milioni 997,300,300. 

Aidha Muro ametoa wito kwa vikundi hivyo kutumia fusra inayotolewa na Serikali kuhakikisha wanapata mkopo wa asilimia kumi ya Makusanyo ya Halmashauri kujikwamu kiuchumi “Mkopo mlioupata leo, ukatumike kwenye malengo husika hasa katika kuwakomboa kiuchumi, kwa kufanya hivyo mtaweza kurejesha na kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kutoka katika umaskini” amesisitiza Muro.

Mwenyekiti wa umoja wa  wanaawake wa CCM ( CWT). BI. Julieth Maturo amepongeza Wilaya hiyo kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM inayoilekeza Serikali kuwainua Wanawake waweze kujikimu kiuchumi ,ambapo ameto wito kwa wanawake waliopata mkopo kuwa na nidhamu ya fedha kwa kutumia fedha hizo kupata maendeleo na kurejesha kwa wakati ili zitolewe kwa vikundi vingine( hatuwezi kupata fedha kwa wakati mmoja ,tutumie fedha hizi kwa maendeleo tujikomboe kiuchumi na tuweze kufanya marejesho na wengine wapate fursa hii”amesisitiza Julieth.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Grace Mbilinyi amesema Halmashauri itaendelea kutekeleza agizo la Serikali la utoaji wa asilimia kumi yamapato ya ndani kwa vikundi vya Wanawake,Vinana na watu wenye changamoto ya ulemavu.

Akisoma taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi hivyo ,Hamson Mrema ambaye ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri hiyo  amesema Halmashauri katika mwaka wa fedha 2019/2020 imetoa mikopo isiyo na riba kwa asilimia miamoja ambapo kiasi cha shilingi milioni 353 zimetolewa kwa vikundi 116 kwa mgawanyo wa  vikundi vya wanawake 99 vilipewa milioni 299 na laki 5 vikundi vya vijana 11 vilipewa milioni 40 na vikindi vya watu wenye changamoto ya ulemavu 6 vilipewa milioni 14.

Aidha Mrema amefafanua fedha zilizotelewa katika hafla hiyo ni sehemu ya fedha za mkopo usio na riba za mwaka wa fedha 2019/2020 ulioishia mwezi juni 2020.

Wanufaika wa mkopo huo wameishukuru Serikali kutoa fursa ya wao kujikwamua kiuchumi ambapo Mwenyekiti wa kikundi cha watu wenye changamoto ya ulemavu kilichonufaika na mkopo huo, amesema wamefarijika kupata mkopo huo kwani utawawezesha kujiendeleza kwenye ufugaji wa kuku na biashara.

Naye Tabu Kisalu ambaye ni miongoni mwa Wanawake walionufaika na mkopo huo ameishukuru Serikali kwa kuwathamini wanawake kwa kuwapa mkopo usio na riba ambao nia asilimia 4 ya mapato ya ndani ya Halmashauri .Pia ametoa wito kwa Wanawake kutumia mikopo hiyo kufanya shughuli za maendeleo na kuwaasa kutotumia fedha hizo kwa mambo yasiyolenga kujikwamua kiuchumi.  Juliana Stephano ambaye ni miongoni mwa vijana walionufaika ametoa Wito kwa vijana kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika Halmashauri kupata kipato na  kujikwamua kiuchumi.

Angelina Christian ambae ni mratibu wa mikopo ametoa wito kwa wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu wanaoomba mkopo katika Halmashauri hiyo kufuata kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo zinazosisitiza vikundi vya Wanawake  kuwa na wanakikundi 10 au zaidi, vikundi vya walemavu kuwa na wanakikundi 5 au zaidi na vijana kuwa na wanakikundi 10 au zaidi.Pia wanakikundi wa vikundi vya vijana wawe na umri wa kuanzia miaka18 hadi miaka 35.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

wanufaika wa mkopo wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.


wanufaika wa mkopo wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Picha ya pamoja ya Mkuu wa Wilay ,viongozi wa Halmashauri naWanakikundi wa kikundi cha watu wenye changamoto ya ulemavu ambao ni miongoni mwa wamenufaika na mkopo  wa Shilingi Milioni 42.

Mwenyekiti wa umoja wa Wanawake ,Wilaya ya kichama Meru Bi.Julieth Maturo akizungumza wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Picha ya pamoja ya Mkuu wa Wilay ,viongozi wa Halmashauri na Wanakikundi wa vikundi vya Wanawake ambao ni miongoni mwa wamenufaika na mkopo  wa Shilingi Milioni 42.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bi.Grace Mbilinyi akisaini hundi ya mfano wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Hamson Mrema ambaye ni Mkuu wa idara ya Maendeleo akitoa taarifa ya utoaji mkopo wakati wa  hafla fupi ya utoaji wa mkopo wa Shilingi Milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 

 Mwenyekiti wa kikundi cha watu wenye changamoto ya ulemavu kilichonufaika na mkopo Ndg.Elirehema Nassary


Juliana Stephano ambaye ni miongoni mwa wanakikundi cha vijana walionufaika na mkopo wa Halmashauri.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa