Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amefanya katika Hospital ya Wilaya ya Meru kwa kupita vitengo mbalimbali na kujionea changamoto zilizopo ili kuzifanyia kazi ikiwa ni mkakati wa uimarishaji wa utoaji huduma bora za afya.
Katika Ziara hiyo Mwl.Makwinya ametoa wito kwa watumishi wa Sekta ya Afya kuendelea kufanya Kazi kwa uadilifu mkubwa kwani Serikali imeweka nguvu kubwa kuboresha Sekta ya Afya Ambapo hivi karibuni imetenga shilingi Milion 550 ikiwa Milioni 300 kwaajili ya ujenzi wa Jengo la dharura katika Hospitali hiyo na Shilingi Milioni 250 ni kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu kilichopo katika Halmashauri hiyo.
Aidha,Mwl.Makwinya amesema ziara hiyo imetoa fursa pia kwa watumishi wa afya kutoa changamoto zinazowakabili ambapo wangelazimika kumfuata Mkurugenzi huyo ofisini.
Kwa upande wa Watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Meru wamemshukuru Mkurugenzi Zainabu kuwatembelea na imekuwa seheme ya kufahamiana .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa