Na Annamaria Makweba
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwl. Zainabu J. Makwinya ametembelea miradi ya Zahanati na Vituo vya Afya katika Halmashauri hiyo kwa lengo la kukagua ujenzi wa miradi ya kuboresha huduma za Afya na mazingira pamoja na kusikiliza kero za watumishi na wananchi katika maeneo hayo.
Katika ziara hiyo iliyohusisha Mradi wa jengo la jengo la Mama na Mtoto pamoja na Mradi wa kuboresha huduma za Afya na Mazingira katika Zahanati ya Mulala Kata ya Songoro, Zahanati ya Maji ya Chai na Kituo cha Afya Mareu Kata ya Kikatiti, Mkurugenzi Makwinya ametoa maelekezo kwa Waganga wafawidhi wa Zahanati na Vituo vya Afya kuhakikisha wanatengeneza mpango wa maendeleo ili kuleta tija katika Jamii.
" Mnatakiwa kuwa na Mpango wa maendeleo ambao utawawezesha kupanga shughuli zenu ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya kuendeleza maeneo haya ya kutolea huduma. " Alisema Makwinya.
Miradi ya kuboresha huduma za Afya na Mazingira iliyokaguli ni pamoja na Shimo la kutupa Kondo, Kichomea, shimo la kutupa majivu, Choo, Stendi ya tenki yenye stoo chini pamoja na kinawia mikono. Ambapo miradi hii ipo katika hatua tofauti za ukamilishaji.
Mbali na kukagua Miradi hiyo, Mwl. Makwinya amesikiliza kero na changamoto mbalimbali za watumishi katika Kata hizo, ikiwa ni pamoja kutopanda daraja ya Mshahara, kutolipwa malimbikizo ya Mshahara pamoja na kutolipwa fedha za uhamisho.
Mwl. Makwinya ametoa maelekezo kwa Waganga Wafawidhi kukusanya taarifa za watumishi wenye madai na kuziwasilisha ofisini kwake ili aweze kuzishughulikia.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji alifuatana na baadhi ya wataalam kutoka Halmashauri ikiwa ni sehemu ya kutoa maelekezo ya moja kwa moja kwa muhusika katika kutatua changamoto hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa