Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo amewataka Waandikishaji Wasaidizi wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5, kufanya zoezi Hilo kwa Uaminifu, Uadilifu , Uzalendo na kuwa na dhamira thabiti .
Mkongo amesema hayo wakati akifunga mafunzo kwa waandikishaji hao Wasaidizi yaliyofanyika kwa siku 3 katika ukumbi wa chuo Cha Mshikamano. Mafunzo hayo yamejumuisha waandikishaji toka Kata 26 na Vituo 53 vya kutolea huduma za afya.
Mkongo amewapongeza kwa kuteuliwa kushiriki katika utekelezaji wa zoezi hilo nyeti na la kihistoria ambapo amewaasa kuwa makini ili kufikia lengo kusudiwa la kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 31,000. "umakini ni muhimu katika zoezi hili ili kuwafikia walengwa ambao ni watoto wa Kitanzania "amehimiza Mkongo.
Aidha, Mkongo ametoa Wito kwa Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kuwahimiza Wananchi wenye watoto wa umri chini ya miaka mitano kujitokeza kuwaandikisha.
Bi. Matha ambaye ni miongoni mwa waandikishaji wasaidizi ameipongeza Serikali kwa kusogeza karibu na Wananchi zoezi la utoaji vyeti kwa watoto bila gharama na kwa muda mfupi baada ya kujiandikisha.
Zoezi la utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 litaanza rasmi tarehe 11Mei 2021 katika Kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Meru pamoja na Vituo 52 vya huduma za afya ambapo vyeti vya kuzaliwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 vitatolewa mara tu baada ya mtoto kuandikishwa katika kituo cha uandikishaji .
Ikumbukwe mzazi/mlezi anapaswa kufika katika kituo cha uandikishaji akiwa na tangazo la kizazi au Kadi ya cliniki ya mtoto ikiwa na majina matatu ya wazazi au cheti cha ubatizo.
Ndg.Emmanuel Mkongo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo .
Restituta Mvungi, Mratibu wa zoezi la uandikishaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya maika 5 akizungumza wakati wa mafunzo.
Wawili kushoto, ni waandikishaji wasaidizi wa vyeti vya kuzaliwa na kulia ni mratibu wa zoezi hilo pamoja na wawezeshaji toka RITA na Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Waandikishaji wasaidizi vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 wakati wa mafunzo.
Waandikishaji wasaidizi vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 wakati wa mafunzo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa