Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bw.Emanuel Mkongo amewaagiza wakuu wa shule za sekondari,walimu wakuu wa shule za msingi,Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri hiyo kuzingatia viwango vya ubora vya ujenzi wa majengo ya Serikali wakati wa utekelezaji wa miradi ya miundombinu mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi.
Aidha Ndg. Mkongo ameeleza hayo wakati wa kikao na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo,"Majengo ya Serikali lazima yawe na ubora na viwango ili kuepuka madhara mbalimbali" amesisitiza Mkongo.
Ndg. Mkongo amewataka wakuu wa Shule za Sekondari, walimu wakuu wa Shule za msingi, Watendaji wa Kata na Vijiji kupata ushauri wa kitaalamu wa viwango vya ubora wa majengo ya Serikali toka kwa mwandisi wa ujenzi wa Halmashauri hiyo kabla ya kutekeleza Miradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa