Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ametembelea Soko jipya la Maji ya Chai kuangalia maendeleo ya Soko hilo.
Mwl. Makwinya ametembelea Soko hilo leo ambalo linatoa huduma ya kuuza mbogamboga, vyakula vya lishe, Matunda na Nguo za Mitumba ambalo lilianza kufanya kazi tarehe 11.06.2023 baada ya kupata ridhaa kutoka Baraza la Halmashauri kuwa Kata ianzishe soko hilo ndipo Halmashauri ianze kutenga Fedha ya kusaidia kuendeleza soko hilo.
Aidha, Diwani wa Kata ya Maji ya Chai, Mhe. Elirehema Mbise amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kufika na kujionea maendeleo ya Soko hilo.
Pia, Mhe. Diwani ameomba msaada kutoka Halmashauri kwa ajili ya kuboresha soko hilo lenye changamoto ya vyoo, miundombinu mibovu ya barabara, Maji pamoja kukosekana kwa kibali cha kuanzisha Mnada katika soko hilo.
Kutokana na changamoto hizo Mkurugenzi Mtendaji ameahidi kufanyia kazi changamoto hizo kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri alioambatana nao katika ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha maombi hayo kwenye kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ili kupata idhini ya kuanza kutenga bajeti ya kuendeleza soko hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa