Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya awapongeza Wananchi wa Kata ya Ambureni kwa ujenzi wa Vyumba vinne (4) vya Madarasa vya Shule ya Sekondari inayotajiwa kuanzishwa January 2022 .
Mwl.Makwinya ametoa pongezi hizo wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo kuona uhalisia , ambapo ameahidi Halmashauri kuunga Mkono jitihada za wananchi kwa kutoa vifaa vya upauzi ikiwemo mbao na bati na kuelekeza ujenzi wa vyoo vya wanafunzi na walimu kuanza mapema .
Vilevile Mwl.Makwinya amempongeza Diwani wa Kata hiyo Mhe. Faraja Maliaki pamoja na viongozi wote wa Kata hiyo kwa kushiriki na kuhamasisha Wananchi Kujiletea maendeleo kwani Kata ya Ambureni ni miongoni mwa Kata mbili (2) za Halmashauri ya Wilaya ya Meru zisizo na Shule za Sekondari. "Nawapongeza Wana Ambureni hakika kazi iendelee"amesema Makwinya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Mhe.Faraja Maliaki amewashukuru wadau na Wananchi kwa michango yao kwenye ujenzi wa Shule hiyo. Pia ameishukuru Halmashauri kwa ahadi ya vifaa vya upauzi na kuomba jitihada za kuhakikisha Shule hiyo inasajiliwa mapema kufanyika kwani wanafunzi wanatembea umbali mrefu kwenda Shule za Kata nyingine.
Aidha, Kata ya Ambureni ni Miongoni mwa Kata saba ambazo Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Juma Makwinya ( katikati)akiwa na Diwani wa Kata ya Ambureni Mhe.Faraja Maliaki pamoja na viongozi wengine wa Kata hiyo.
Ujenzi wa Vyumba vinne (4) vya Madarasa vya Shule ya Sekondari inayotajiwa kuanzishwa January 2022 katika Kata ya Ambureni.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa