Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo aripoti rasmi kwenye Halmashauri hiyo tayari kuanza uteelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi Mkongo amewasili ofisini leo tarehe 20 Agosti 2018 baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 13 Agosti 2018 .
Mkongo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro pamoja na kaimu Mkurugenzi ambaye ni mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Grace Mbilinyi
Mkongo akizungumza na wakuu wa idara na vitengo, ameweka bayana dira ya uongozi wake ni kuisimamia vyema Halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria, kampuni, taratibu ambapo atajikita kwenye ukusanyaji wa mapato yatakayotumika kuiendesha Halmashauri hiyo na kuleta maendeleo kwa wananchi
Mkongo amewaasa wakuu hao wa idara na vitengo kufanya kazi kwa ushirikiano na kutekeleza majukumu yao ipasavyo pamoja na kuwasimamia vyema watumishi walio chini yao sambamba na kuzingatia taaluma zao kutoa ushauri utakaoleta tija katika Halmashauri hiyo .“sitegemei kupewa taarifa isiyo sahihi na afisa wa Halmashauri hii” amesisitiza Mkongo.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa idara na Vitengo Afisa elimu wa Sekondari, Mwl. Damari Mchome amempongeza Mkurugenzi Mkongo kwa kuteuliwa, pia ameeleza wapo tayari kumpa ushirikiano .
Kabla ya uteuzi wa Mkurugenzi Emmanuel Mkongo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilikuwa inaongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi Ndg. Christopher Kazeri .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo akisisain Kitabu cha maudhirio.
Kikao cha kufahamiana kati ya Mkurugenzi Mtendaji WA Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo na wakuu wa idara na vitengo .
Kikao cha kufahamiana kati ya Mkurugenzi Emmanuel Mkongo na wakuu wa idara na vitengona wakuu wa idara na vitengo.
Kikao cha kufahamiana kati ya Mkurugenzi Emmanuel Mkongo na wakuu wa idara na vitengo.
Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza Mkurugenzi Mkongo wakati wa kikao cha kufahamiana.
Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza Mkurugenzi Mkongo wakati wa kikao cha kufahamiana.
Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza Mkurugenzi Mkongo wakati wa kikao cha kufahamiana.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro pamoja na kaimu Mkurugenzi ambaye ni mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Grace Mbilinyi na Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Meru pamoja na wajumbe wengine.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa