MKUTANO WA 4 WA WIKI YA UFUATILIAJI, TATHIMINI NA UJIFUNZAJI (MEL) MKOANI MWANZA
Imewekwa: September 12th, 2025
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ameendelea kushiriki Mkutano wa 4 wa Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Ujifunzaji (MEL) unaofanyika katika Ukumbi wa Malaika Resort jijini Mwanza.
Mkutano huo ni jukwaa muhimu linalowawezesha wataalamuu, watunga sera, watafiti na watekelezaji kubadilishana maarifa na mbinu bora za kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini nchini.
ambapo Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu (PMO-PPC) kwa lengo la kuimarisha umiliki wa ndani wa mifumo ya MEL na kujenga mazingira endelevu ya tathmini. Aidha, unalenga kuongeza uelewa na mshikamano katika kukuza matumizi ya ushahidi katika uundaji sera na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Mkutano wa 4 wa Wiki ya MEL unasistiza ajenda kuu tatu: kuimarisha mifumo ya MEL katika ngazi za kijamii, kikanda na kitaifa, kukuza matumizi ya ushahidi katika uundaji sera na utoaji huduma bora, pamoja na kuhamasisha ushirikiano katika ufadhili na maendeleo ya taasisi zinazojihusisha na MEL.