Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Grace Mbilinyi amewataka watumishi wa idara hiyo kutokufanya kazi kwa mazoea.
Mkuu huyo wa Idara ya utawala amesikitishwa na uwepo wa baadhi ya watumishi ambao hawajakamilisha ujazaji wa fomu za mfumo wa wazi wa mapitio na tathimini ya utendaji kazi (OPRAS)mwaka 2017/2018 na 2018/2019 ,ambayo humwezesha mtumishi kupanga malengo na kuwajibika .
Akizungunza wakati wa kikao cha watumishi wa Idara hiyo, Grace Mbilinyi amewaagiza watumishi ambao hawajakamilisha ujazaji wa fomu za OPRAS kukamilisha mara moja, pia amewaonya watumishi wanaochelewa kwenye vituo vyao vya jazi kuacha tabia hiyo kwani ofisi yake haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu. “ nguzo ya kutekeleza majukumu yenu ni kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma” Ameeleza Grace Mbilin yi.
Blandina Denis ambaye ni Mtendaji wa Kijiji cha Nrumangeny ameipongeza Idara hiyo kwa kuitisha vikao hivyo vyenye tija kwenye utendaji na uwajibikaji wa mtumishi pamoja na kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu.
Aidha Idara ya Utawala na Rasilimali watu imekuwa ikitoa ufahamu na elimu juu ya ujazaji wa fomu za OPRAS pale mtumishi anapoajiriwa na watumishi ukumbushwa mara kwa mara kupitia vikao vya idara .
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkuu wa idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Grace Mbilinyi akizungumza wakati wa kikao cha idara hiyo.
Afisa Utumishi Edward Chitete (kulia) na Afisa Utumishi Lucy Kira ,wakati wa kikao cha idara.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wakati wa kikao cha Idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wakati wa kikao cha Idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wakati wa kikao cha Idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wakati wa kikao cha Idara hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa