Kwenye mkutano wa hadhara ya wananchi katika uwanja wa mpira Ngarasero Usa-River mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wananchi kutovaamia mashamba kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria,hayo ameeleza alipokua kwenye ziara yake ya siku moja wilayani Arumeru kwenye Halmashauri ya Meru akijibu hoja iliyotolewa na Ramadhani Mwinyi mkazi wa Usa-River ya wananchi kutohusishwa kwenye mgao wa mashamba yanayofutiwa hati miliki na Serikali na kupelekea ugawaji huo kuwa na upendeleo.pia ameagiza wananchi kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ugawaji ardhi.
Nao wananchi wa kia kijiji cha Kolila kata ya Malula wamemuomba mkuu huyo wa mkoa kutafuta ufumbuzi wa sitofahamu ya mpaka kati ya Mkoa wa kilimanjaro na Arusha kwani umekua ukiadhiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ikiwemo ukusanyaji wa kodi ,mkuu huyo wa mkoa ametoa ahadi ya kuchangia kiasi cha laki tano kwaajili ya ujenzi wa shule ya msingi utakapo anza katika kijiji hicho cha ikumbukwe kua Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli imetoa kipaumbele kikubwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini
Katika ziara hiyo kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi zilitolewa ufafanuzi na majibu na nyingine kwa kuzingatia umakini baadhi ya kero zitafanyiwa kazi katika ofisi ya mkuu wa mkoa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mhe.Rais Dk. John Magufuli aliposimamwishwa na wananchi akielekea uwanja wa ndege kia baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 kuanzia tarehe 20-23/09/2017 mkoani Arusha
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa