Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Iddi Kimanta amezindua miradi katika sekta ya Kilimo na Elimu yenye thamani ya zaidi ya ya Milioni 820 iliyofadhiliwa na kutekelezwa na shirika la World Vision katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wilayani Arumeru.
Ndg. Alphonce Krarija kutoka shirika hilo ameitaja mradi hiyo kuwa ni kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Shambarai ambao umegharimu jumla ya shilingi Milioni 422 na miradi yenye thamani ya shilingi Milioni 406 katika shule ya Msingi kerikenyi ya ujenzi wa Nyumba ya Walimu (two in one), ujenzi wa vyoo vya wanafunzi vyenye matundu 20, tanki la kuhifadhia Maji na karo la kunawia mikono.
Aidha, Kimanta amepongeza shirika hilo na kuwataka Wananchi kulinda na kuisimamia miradi hiyo "hakuna haki bila wajibu " amehimiza Mheshimiwa Kimanta.
Pia, Kimanta ameahidi kuchangia ujenzi wa ofisi ya Walimu katika shule ya Msingi Kerikenyi kwa kutoa tofali 1,500 na Mkuu wa Wilaya kutoa saruji. Aidha, Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru umeahidi kuchangia vifaa katika hatua za ukamilishaji.
Mkuu wa Mkoa amehitimisha kwa kuwaagiza wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi ili kuongea ari ya wanachi katika kuchangia miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ameahidi kuendelea Kushirikiana na wadau pamoja na Wananchi kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na tija.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya amepongeza utendaji wa Serikali katika jitihada za kuinua Wakulima kiuchumi.
Aidha, katika ziara hiyo Mheshimiwa Kimanta aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkurugenzi wa Wolrd Vision Tanzania, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo pamoja na Wataalam ngazi ya Mkoa,Wilaya na Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa