Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amesema Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuleta fedha nyingi za maendeleo katika Halmashauri 7 za Mkoa huo ambapo amehimiza miradi kukamilika kwa wakati ili kuwa na tija iliyokusudiwa " Serikali inafanya jitihada kubwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kutoa fedha za miradi hivyo kamilisheni miradi kwa wakati na kwa ubora "amehimiza Mhe.Mongela
Mhe.Mongela amesema hayo wakati akikagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Kikwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Wilayani Arumeru ambapo Serikali imetatua changamoto ya uhaba na uchakavu wa vyumba vya madarasa kwa kutoa milioni 60 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule hiyo ilijengwa toka mwaka 1974.
Mhe.Mongela ameupongeza uongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa Ushirikiano mzuri na wadau wa maendeleo ambapo mwekezaji RIJKZWAAAN QSEM alichangia milioni 163 katika ukamilishaji wa Zahanati ya Maksoro ambayo imekamilika kwa milioni 180 ikiwa ni pamoja na mchango wa wananchi na inatarajiwa kuhudumia watu 600 wa kijiji cha Maksoro na Vijiji vya Jirani.
Kipekee Mhe.Mongela amemshukuru Mhe.Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuamsha ari ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Kikatiti uliosimama kwa takribani miaka tisa toka kuanza kujengwa mwaka 2013 ambapo Oktoba 2021 Mhe.Rais Samia wakati akisalimiana na wananchi wa Kikatiti alichangia Milioni 10 za ukamilishaji wa Zahanati hiyo na kuchochea Halmashauri kuchangia Milioni 10 ,Mbunge kupitia mfuko wa Jimbo Milioni 5 na shirika la CTSI milioni 128.
Vilevile Mongela amesema Serikali imejikita kuwaletea wananchi wake maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya, Maji , Barabara nk ambapo ameelekeza kutekeleza miradi kwa taratibu na ubora sambamba na kutumia njia shirikishi .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa Kikwe wameishukuru Serikali kutoa milioni 60 za ujenzi wa madarasa matatu ambapo Mkuu wa Mkoa ameongoza uchangiaji wa mifuko 380 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mengine"Hii shule imejengwa inakaribia miaka 50 toka imejengwa madarasa ni machache na mengine yamezeka hivyo Serikali imetupa milioni 60 ya madarasa matatu na Mkuu wetu wa Mkoa kutuwezesha kupata mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madara mengine tunashukuru sana "amesema Joel Mbise mkazi wa Kikwe
Katika ziara hiyo Mhe .Mkuu wa Mkoa akiambatana na Viongozi wa Chama na Serikali kuanzia ngazi ya Mkoa alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Amsha na Mradi wa Usambazaji Maji Patandi.
Baadhi ya picha za tukio
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela (mwenye kofia), Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango (wa lwanza kulia) Mkurigenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya na Mkurugenzi wa shirika la CTSI Bw.Kim
Muonekano wa Zahanati ya Kikatiti
Muonekano wa Mbele wa Zahanati ya Kikatiti
Kinamama wa Kikatiti wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati wa Ziara.
Ukagunzi wa tenki la kuhifadhia maji katika mradi wa usambazaji maji Patandi
Ukamilishaki wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Samaria.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa