Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo atatua Changamoto zinazoikabili Halmashauri ya Wilaya ya wila ya Meru ametatua changamo hizo alipohudhuria kikao cha baraza la Waheshimiwa madiwani Tarehe 02 Mei 2017 .
Mkuu huyo wa mkoa amejibu hoja ya ukosefu wa maeneo kwaajili ya ofisi za kijiji na kata kwa kuwataka viongozi kuhakikisha ardhi katika maeneo yao haiuzwi kiolela na kupeleke ukosefu wa Ardi kwa matumizi ya shughuli za kijamii na matumizi mengine kwa maendeleo ya wananchi kwa kutoa mfano wa fursa ya mradi wa ujenzi wa bandari ya nchi kavu unaotarijiwa kufanyika ndani ya Halmashauri ya Meru utakaohitaji eneo la ukubwa usiopungua hekari 500.
Katika kutaua changamoto ya posho kwa waheshimiwa madiwani amewaagiza wakurugenzi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwalipa madiwani posho kutokana na stahiki zao akitoa angalizo la posho na matumizi ya fedha kwa kufafanua fedha zote za mapato ya Halmashauri ni Mali ya wananchi na si vinginevyo hivyo zitumike kwa kuzingatia taratibu. Agizo hilo kwa wakurugenzi ni pamoja na kuhakikisha wanatenga asilimia 10% ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa