MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AFANYA KIKAO NA UONGOZI WA JMAT
Imewekwa: September 11th, 2025
Mapema hii leo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Mwinyi Ahmed Mwinyi amefanya kikao kifupi cha utambuzi wa viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) ngazi ya wilaya na kata, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meru.
Mheshimiwa Mwinyi Ahmed Mwinyi akizungumza na viongozi hao amesema Mkoa wa Arusha kwa unatarajia kumpokea mheshimiwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan hivyo amewataka kushirikiana wote kwa pamoja kumpokea mheshimiwa Raisi lakini pia kuendelea kuhimiza udumishaji wa Amani na mshikamano katika maeneo yetu yote yanayotuzunguka
Aidha katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewahimiza viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kuzidi kuweka mikakati ya kulinda na kuimarisha amani wakati Taifa linaelekea katika kipindi cha uchaguzi