Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro leo amepata fursa, kujitambulisha kwa watumishi wa Halmashauri ya Meru , utambulisho huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya,ametambulishwa kwa watumishi wa Halmashauri hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Kimanta aliyekuwa akikaimu Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwa takribani miezi nane .
Mheshimiwa Muro baada ya kutambulishwa amewatoa hofu watumishi hao kuwa ujio wake utawapa ushirikiano na kuwawezesha kutimiza majukumu yao ikiwa ni utoaji wa huduma bora ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi pamoja na rasilimali za Tanzania kuwanufaisha wananchi wote hasa wanyonge na watoto wa maskini, nukuu "nimekuja hapa kutimiza torati na si kuivunja".
Ameongeza kuwa ushirikiano huo utaanza kwa kuwapa fursa watumishi hao kueleza changamoto zao na kupokea mawazo,maoni na mikakati itakayoleta maendeleo kwenye Halmashauri hiyo na Wilaya ya Arumeru katika kikao kinachotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 6 Agosti 2018.
Naye mkuu wa Wilaya ya Monduli, baada ya kumtambulisha mkuu huyo mpya wa wilaya ya Arumeru, alitamka kumkabidhi watumishi wa Meru wakiwa weupe, wenye afya njema, wanyenyekevu na wachapakazi na kuwataka watumishi hao, kumpa ushirikiano mkuu huyo wa wilaya kama walivyompa yeye.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Arumeru mheshimiwa Jerry Muro, ameanza kazi rasmi ya kuwatumikia wana Arumeru baada ya kuapishwa jana na mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Mrisho Gambo mara baada ya kuteuliwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki iliyopita.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO
Mkuu wa Wilaya ya Monduli mheshimiwa Idd Kimanta akizungumza wakati wa kikao.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye kikao .
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye kikao .
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na watumishi wa asasi nyingine za Serikali wakiwa kwenye kikao .
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye kikao .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa