Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa wito kwa wafanyabiashara wa soko la Tengeru katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha wanahesabiwa katika Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022 ambapo makarani wa Sensa watapita kwenye kila kaya kuhesabu watu.
Aidha ,Mhe Ruyango amesema sensa ina manufaa makubwa kwani Serikali itatumia takwimu za sensa kwenye kupanga na kuboresha huduma za kijamii kama vile uboreshaji wa miundombinu ya masoko, vituo vya huduma za afya nk "nimekuja hapa sokoni niwakumbushe kutoa taarifa sahihi zitakazoisaidi Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia idadi halisi ya watu" amehimiza Ruyango
Mtakwimu Ismail Issa ambaye ni Mratibu wa Sensa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema watu watakao hesabiwa siku ya sensa tarehe 23 Agosti 2022 ni wale wote waliolala hapa nchini usiku wa kuamkia tarehe 23 Agosti 2022 hivyo ametoa wito kwa wakuu wa Kaya kuwa na taarifa za watu wote waliolala kwenye kaya zao usiku wa kuamkia siku ya sensa.
Bw.Hamisi Juma mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Meru ambaye ni mwenyekiti wa chama cha CUF ametoa wito kwa wananchi wa vyama vyote vya Siasa kushiriki zoezi la Sensa tarehe 23 Agosti 2022 ili Nchi ipate takwimu sahihi zitakazotumika kuleta maendeleo "maendeleo hayana chama hatuna budi kushiriki zoezi hili la Sensa kwa kutoa taarifa sahihi "amehimiza Hamisi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake wafanya biashara wa soko la Tengeru wameipongeza Serikali kwa namna inavyohakikisha Elimu ya Sensa inawafikia wananchi katika maeneo yao na kuahidi kuhakikisha wanashiriki maendeleo ya nchi kwa kuhesabiwa katika zoezi la sensa " sisi kinamama tupo tayari kuhesabiwa na tunawasihi wengine wote kushiriki zoezi la sensa " amesema Grace Akyoo
SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Tengeru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa