Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel J. Mkongo amekabidhi tena, fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa Bi. Evaline Kaaya kupitia Chama cha NCCR Mageuzi.
Aidha Msimamizi huyo wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Mgombea huyo amekabidhiwa fomu hiyo, kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, iliyopo kwenye Ofisi za Makao Makuu Halmashauri ya Meru.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel J. Mkongo akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge kwa Evaline Kaaya wa Chama cha NCCR Mageuzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa