Wananchi wa Manyata Kata ya Usa - River ,Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamepokea kwa shangwe na nderemo mradi wa kukarabati barabara ya Manyata - Nganana urefu wa Km 5.7.
Aidha mradi huo wa ukarabati wa barabara ya Manyata - Nganana utagharimu fedha kiasi cha Tsh.64,919,458.01 ambazo zimeidhinishwa na Serikali kupitia Mfuko wa TASAF .
Wananchi hao wameeleza kuwa ukarabati wa barabara hiyo ya Manyata - Nganana utasaidia watoto kuhudhuria shule na kupata elimu bora pia utaboresha huduma za afya,kurahisisisha usafiri wa mazao ya kilimo na wakazi sambamba na kuongeza kipato kwa Walengwa wa TASAF III ambao watashiriki kufanya shughuli za kibinadamu katika mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro amewataka wasimamizi wa mradi huo wa ukarabati wa barabara Manyata - Nganana kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha yana zingatiwa "fedha ya TASAF ni mbegu inafaa ipandwe izae matunda hivyo mbegu huwa hailiwi" amesisitiza Mhe. Muro.
Nae Mratibu wa TASAF katika Halmashauri hiyo Ndg.Boniface Mwilenga amesema asilimia 88 ya fedha za mradi huo wa ukarabati wa barabara ya Manyata - Nganana km 5.7 sawa na Tsh.57,778,317.63 zitatumika kutekeleza mradi wenyewe, huku asilimia 12 sawa na Tsh. 7,141,140.38 zitatumika kwa ajili ya usimamizi kuanzia ngazi ya kijiji,Kata na Halmashauri.
Mwilenga ameongeza kuwa katika fedha hizo Tsh.57,778,317.63 ambazo ni za utekelezaji wa mradi wenyewe kiasi cha Tsh.28,889,158.82 zitatumika kununua vifaa vya ujenzi huku kiasi kilichobaki Tsh.28,889,158.82 zitatumika kuwalipa ujira walengwa wa TASAF watakao kuwa wanafanya kazi.
Aidha kwa mujibu wa Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Meru Utekelezaji wa TASAF unaitambua Manyata kama kijiji chenye vitongoji viwili vya Manyata kati na Nganana.
Kwa sasaManyata ni miongoni mwa vitongoji vinavyounda mamlaka ya mji mdogo Usa -River katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wananchi wa Manyata wakicheza kwa furaha kabla ya uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro akizungumza na wananchi wa Manyata wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata - Nganana.
Mratibu waTASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Ndg.Boniface Mwilenga akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati barabara ya Manyata - Nganana.
Wananchi wa Manyata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Mhe.Diwani wa Kata ya Usa - River akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata - Nganana.
Wananchi wa Manyata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Wananchi wa Manyata wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ukarabati wa barabara ya Manyata -Nganana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa