Ikiwa zimebaki Siku Mbili Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mapema hii Leo Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya amezungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyo shiriki Uchaguzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kwa Lengo la kukumbushana kuhusu kuendelea kusimamia kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa
Aidha Mwl. Makwinya ameendelea kuwapongeza viongozi hao kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kusimamia kanuni na taratibu zilizowekwa na kutoa Taarifa za haraka Kwa changamoto zozote zinazojitokeza.
Pia kikao hiko kilikuwa na Lengo la kuwajulisha viongozi hao juu ya Vituo vya kupigia Kura 13 vilivyo ongezeka na kuwataka kuandaa mawakala watakaoapishwa kwa ajili ya kusimamia katika vituo hivyo.
Msimamizi wa Uchaguzi ameeleza kuwa wakati wa kuanza zoezi la Uchaguzi vyama 17 vilijitokeza kugombea nafasi mbalimbali lakini hadi zoezi la kuingia kwenye kampeni ni vyama 13 vitashiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mwl. Makwinya amemaliza kwakusema njia ya Kutatua changamoto niyakukaa mezani na kuzungumza hivyo amewaomba kadri changamoto yoyote inayojitokeza basi apewe Taarifa ya haraka ili kuweza Kutatua changam oto hizo na Wananchi wapatiwe huduma na stahiki Yao ya kushiriki Uchaguzi wa Amani na salama.
Viongozi wa Vyama vya Siasa vilivyoshiriki kikao hicho ni pamoja na Chama cha Mapinduzi(CCM), TLP, DP, ADC, DP, SAU, AAFP, ACT, Demokrasia Makini, UMD na CHAUMA huku Chama cha CCK na CHADEMA kuomba udhuru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa