Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel J. Mkongo amemkabidhi rasmi, fomu za Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa Ndg.Simon P. Ngilisho kupitia Chama cha Demokrasia Makini (DM).
Mgombea huyo wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini (DM), amekabidhiwa fomu hizo, mnamo saa 09.21 Alasiri, kwenye Ofisi ya Msimamizi Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki, iliyopo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi, amemkabidhi fomu ya Uteuzi kwa mgombea huyo, kufuatia Maelekezo ya Fomu ya Uteuzi Na. 8B, kwa mujibu wa Kifungu cha 38 (3) na (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ikiweka wazi mambo yaliyojumuishwa kwenye fomu ya Uteuzi.
Ndg.Simon P. Ngilisho kupitia Chama cha Demokrasia Makini , amekuwa Mgombea wa kwanza kuchukua fomu ya Uteuzi wa Ubunge kwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki , Emmanuel J. Mkongo (kulia) akimkabidhi fomu ya Uteuzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru mashariki Ndg.Simon P. Ngilisho kupitia Chama cha Demokrasia Makini DM. kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo mnamo saa 9.21 mchana wa leo
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini DM Ndg.Simon P. Ngilisho baada ya kukabidhiwa fomu ya uteuzi wa kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini DM akisaini kitabu cha kukiri kupokea fomu ya Uteuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arumeru Mashariki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa