Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilipokea kiasi cha shilingi 584,280,029.00 kutoka program ya kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Karangai Kata ya Kikwe.
Serikali imetoa fedha hizo ili Kujenga shule kwenye Kata hiyo kwa lengo la kupunguza changamoto iliyopo ya kutokuwa na Sekondari katika eneo hilo na kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali mrefu ili kuweka huduma hiyo karibu pia kuwezesha shule hiyo kupokea wanafunzi mwaka 2025.
Waheshimiwa Madiwani na Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango wamefanya ziara katika eneo hilo ili kuangalia zoezi na hatua iliyofikiwa. Ziara ambayo ni ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024 kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Pia, TAMISEMI imetoa mwongozo wa orodha ya utekelezaji wa program hiyo ya ujenzi wa shule mpya ikiwa ni ujenzi wa jengo lenye vyumba vya Madarasa 8 na ofisi 2, jengo la Utawala, jengo lenye Maabara ya Kemia, Fizikia na Bailojia, Jengo la Maktaba, Chumba cha TEHAMA, jengo la vyoo vya wanafunzi wavulana lenye matundu 8 na Matundu 8 kwa Wasichana yakiwa na huduma kwa wenye mahitaji maalum, Kichomea taka, pamoja na Tanki la maji la ardhini.
Katika utekelezaji wa mradi huo wa uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Ujenzi umeanza na upo hatua ya kuchimba Msingi.
Wajumbe hao wametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kata ya Kikwe.
" Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa