Tarehe 04 Septemba 2017 Halmashauri ya Meru ilipokea mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Arusha na kuukimbiza katika tarafa zote tatu (Poli,Mbuguni na King’or) kwa urefu wa kilometa 92 ,umbali kutoka kituo cha mkesha wa Mwenge huu wa Uhuru hadi eneo la Makabithiano ulikua urefu wa kilometa 11 hivyo kufanya mbio hizi kua na umbali wa kilometa 103.
Aidha mbio hizi miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 2,099,898,688.18 iliwekewa jiwe la ufunguzi/msingi na kiongozi wa mbio za mwenge Ndg.Amour Hamad Amour ,
Aidha miradi ipatayo sita iliyozinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi ni kama ifuatavyo ,miradi iliyofunguliwa ni mradi wa kuhifadhi mazingira Nkoanekoli ,katika uzinduzi wa Mradi huu kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg,Amour Hamad Amour aliipongeza Halmashauri ya Meru kwa kua mshindi wa kwanza kitaifa katika kampeni ya usafi na mazingira kati ya Halmashauri za wilaya ,pia alipongeza utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu uliowezesha walengwa kua na mradi huu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa