Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro, anawatangazia wananchi wote kushiriki katika Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 katika wilaya ya Arumeru.
Mwenge wa UHURU 2021 utawasili katika Wilaya ya Arumeru siku ya Ijumaa, tarehe 19.06.202, katika eneo la Mlangarini kwa Robert na kukimbizwa umbali wa Kilomita 126.3, katika halmashauri mbili za Arusha na Meru, na kupitia kwenye miradi tisa (9), yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3 katika sekta ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na Uwekezaji.
MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE MAALUM WA UHURU 2021 NI PAMOJA NA:-
1.MRADI wa TEHAMA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI.2
2.MRADI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA KIKWE.
3. MRADI WA BARABARA SANGISI - NAMBALA KATA YA ALHERI
4 MRADI UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA -OLOIRIENI
5. MRADI WA KUSUKUMA MAJI LOSIKITO
6. MRADI WA SHAMBA LA MIGOMBA NA TUMBAKU OLTURUMET
7 MRADI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA WILAYA OLTURUMET
8. MRADI WA MIUNDOMBINU YA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM SHULE YA MSINGI ILBORU
9. MRADI WA KIKUNDI CHA VIJANA – UMOJA YOUTH GROUP MOIVO.
MWENGE WA UHURU 2021 UTAKESHA KATIKA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA ARUSHA ENEO LA SEKEI.
NYOTE MNAKARIBISHWA✍✍✍
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2021 “TEHAMA ni Msingi wa Taifa endelevu; itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa