Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili ametoa maelekezo kwa Kamati mpya zilizochaguliwa kuhakikisha kuwa wanakwenda kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa Katika Halmashauri na kuzitafutia ufumbuzi.
Mhe. Kishili amesema hayo wakati akihitimisha Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Halmashauri uliokuwa na ajenda ya Kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Kuteua wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri kwa mwaka 2024/2025, kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na kupitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri kwa mwaka 2024/2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa