Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Mhe.Will Njau Kabla ya ufunguzi wa kikao cha kamati ya fedha ,Utawala na Mipango, ameeleza kuridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Mkongo ambapo ametoa wito kwa wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo kumpa ushirikiano.
Mhe.Njau amesema ufanisi wa kazi ni sambamba na ushikiano baina ya wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani na wataalamu "Ushirikiano ni jambo muhimu kwenye Maendeleo ya Halmashauri " amesisitiza Mhe.Njau.
Mhe.Njau ameongeza kuwa utendaji wa Mkongo ni tumaini kubwa kwa maendeleo ya Halmashauri hiyo kwani kwa kipindi kifupi alichofika kwenye Halmashuri hiyo ameweza kutatua changamoto zilizokuwa zinakwamisha maendeleo ya Halmashauri hiyo ikiwemo vibali vya michango ya kutekeleza miradi iliyoibuliwa na Wananchi kwenye Kata na Vijiji.
Nae MKurugenzi Mkongo wakati akijitambulisha ameweka wazi ujio wake kwenye Halmashauri ya Meru ni kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kutatua kero zinazowakabili wananchi na kueleza kuwa yupo tayari kushirikiana na madiwani katika swala la maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Kikao hicho cha Kamati ya fedha ,Mipango na utawala kimekua fursa kwa Mara ya kwanza Kwa MKurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru ,Emmanuel MKongo kutambulishwa rasmi kwa Madiwani toka aripoti kwenye Halmashauri hiyo tarehe 20 Agosti 2018.
PICHA ZA TUKIO.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ,Mhe.Willy Njau akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Fedha ,Utawala na Mipango.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru akimkaribisha na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru akimkaribisha na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo akizungumza na wajumbe wa kamati ya Fedha ,utawala,na Mipango.
Wajumbe wa kamati ya Fedha ,utawala,na Mipango ambao ni madiwani wakati wa utambulisho.
Wajumbe wa kamati ya Fedha ,utawala,na Mipango ambao ni madiwani wakati wa utambulisho.
Wajumbe wa kamati ya Fedha ,utawala,na Mipango ambao ni wataalamu wakati wa utambulisho.
wajumbe wakamati ya Fedha ,utawala,na Mipango ambao ni wataalamu wakati wa utambulisho.
KUPATA TAARIFA,MATANGAZO NA HABARI MBALIMBALI TOKA HALMASHAURI YA MERU NA SERIKALI KUU TEMBELEA TOVUTI YA HALMASHAURI www.merudc.go.tz.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa