Leo Watumishi wa Halmashauri ya Meru ,Ndugu ,jamaa na marafiki wajitokeza kwa wingi kuuaga Mwili wa aliyekua Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Majengo Dr.Herman Ladislaus Ngalika aliyefariki baada ya kupata ajali ya Pikipiki iliyotokea tarehe 15 Novemba 2017 maeneo ya Mshikamono,tukio hilo la kuaaga mwili wa Marehemu Dr.Herman limefanyika katika Hospitali ya Wilaya Tengeru likiongozwa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Meru Dr. Cosmas Kilasara
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Hamson Mrema ambaye ni mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii amesema Halmashauri inasikitika kumpotenza mtumishi wake pia ametoa pole kwa Familia,Ndugu ,jamaa na marafiki na kuwatakia safari njema katika kuupeleka mwili wa Marehemu Mkoani Morogoro ambako ndiko nyumbani kwao kwaajili ya mazinko ,Bwana ametoa bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa