Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Mwl. Zainabu Makwinya mapema hii Leo amefungua Semina Kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Aidha Mwl. Makwinya amewataka wasaidizi hao waliopata dhamana ya kwenda kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha Upatikanaji wa Viongozi Bora katika Maeneo watakayo pangiwa na kuwataka kusimamia haki panapostahili haki. Mwl. Makwinya ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze kushiriki Uchaguzi "
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa