Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamkaribisha rasmi Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo kwa kumtunuku zawadi mbalimbali kama ishara ya kumpa ushirikiano na Umoja .
Miongoni mwa watumishi hao wamemshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwaamini Wanawake ambapo amemteua Mwl.Zainabu Makwinya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, "Wanawake tunajivunia kuwa na Mkurugenzi Mwanamke hii inatutia moyo na kuongeza bidii ya kuchapa Kazi" amesema Digna Masawe, Afisa kilimo Halmashauri hiyo
Pia.Watumishi hao wamemuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Emmanuel J.Mkongo kwa kumtunuku zawadi kama alama ya uchapakazi wake katika Halmashauri hiyo
KatikaHafla hiyo fupi ya kuaga na kukaribisha,Watumishi hao wamemkaribisha pia mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Ndg.Arnold Buretta pamoja kumwaga mtangulizi wake Bi.Grace Mbilinyi pamoja na Aliyekuwa Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Bw. Maarufu Mkwaya.
Mwl.Zainabu Makwinya,Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa