Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso , ameagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru kuwashikilia na kuwaweka chini ya ulinzi viongozi watatu wa bodi ya Maji MAKILENGA Halmashauri ya Meru,Wilayani Arumeru kwa tuhuma za kufanya ubadhirifu kwenye Mradi huo.
Aweso ametoa agizo hilo baada ya kubaini uwepo wa ubadhirifu wa fedha za mradi huo licha ya makusanyo ya fedha zinazotokana na uchangiaji wa huduma ya maji kufika kiasi cha milioni tano (5) kila mwezi bodi imebakiwa na kiasi kisichozidi milioni moja na nusu tu, “Haiwezekani asilimia kubwa ya mradi unatumia vyanzo vya mtiririko matumizi yake kuwa makubwa kiasi cha kumaliza fedha zote za miaka minne”amehoji Aweso.
Waliokamatwa kwa tuhuma za kuhujumu mradi huo ni pamoja na mwenyekiti wa Bodi Godhope Chales,Mhasibu wa Mradi Bi.Warialanga Pallangyo,pamoja na fundi bomba wa mradi huyo anayetambulika kwa jina la Kaaya.Meneja wa Mradi huo Orest Manyanga amewekwa chini ya ulinzi kwa kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa kikao cha Naibu waziri na wajumbe wa bodi ya MAKILENGA.
Aidha Aweso ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Maji Kiiji cha Kingori wenye thamani ya Shilingi bilion 1.5 sambamba na kumpongeza mkandarasi kwa utendaji mzuri chini ya usamizi wa Uongozi wa Wilaya hiyo.
Haya yamejiri wakati wa ziara ya Naibu huyo Wilayani Arumeru iliyolenga kutembelea na kukagua Miradi ya Maji ili kuweza kutambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa Miradi ya maji kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza mpaka kufikia 2025 upatikanaji wa maji vijijini kuwa asilimia 85 na mjini 95.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akieleza namna Wilaya hiyo inavyosimamia utekelezaji wa Miradi ili wananchi waweze kunufaika.
Mhe.Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki John Pallangyo akiishukuru Serikali kusikia kilio alichowasilisha Bungeni cha wananchi Wameru kuhusu maswala ya Maji kilichopelekea Naibu waziri wa Maji kufanya ziara Wilayani hapo ili kutatua changamoto hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,Nelson Mafie ameipongeza Serikali kwa utatuzi wa changamoto za wananchi ambapo imeunda chombo cha wakala wa maji vijijini na Mjini (RUWASA)."huu ndio Mwarubaini wa changamoto za ya maji "amesisitiza Mafie.
Wananchi wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kutumia fedha zake kugharamia kumsafirisha Mzee Senyaeli Mbise Maarufu kama Lemali, ambaye ni fundi mwenye uelewa wa mradi wa Maji MAKILENGA kurudi kuendelea na kazi hiyo baada ya fundi aliyekuwepo kuwa kikwazo kwenye utendaji.
Wajumbe wabodi ya MAKILENGA,viongozi na wanachi na wataalamu wakifuatilia kikao
viongozi na wanachi na wataalamu wakifuatilia kikao
Viongozi na wananchi wa Kata ya Kingori wakifuatilia kikao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa