• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI aridhishwa na ujenzi wa shule Bora ya mfano Nchini.

Imewekwa: January 14th, 2021

Mhe.David Sindile  waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI  (Mb) ameridhishwa na ujenzi wa shule  ya Sekondari ya Mfano nchini ya Patandi maalum iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru.

Haya yamejiri wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotelelezwa kwa Mpango wa Lipa kutokana na Matokeo (EP4R) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru  ambapo amepongeza ujenzi wa shule ya Sekondari ya Patandi maalum iliyogharimu zaidi ya Bilioni 3.

Mheshimiwa Silinde  ameeleza kuwa Serikali mbali na kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mpango wa EP4R  imeweka mikakati ya kuendelea   kuboresha  sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya kufundishia  na kujifunzia kwa kuanza ujenzi wa shule za Sekondari 1000 .

Aidha, Silinde amesema ujenzi wa shule hizo 1000  utafanyika  kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza shule 154 zitajengwa.

Mhe. Silinde amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro kwa usimamizi wa miradi Wilayani humo sambamba na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Meru  na Arusha kwa ubunifu na utendaji kazi wenye tija katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa na utekelezaji wa Miradi ya P4R .

Naye Mhe.Dkt.John D. Pallangyo,  Mbunge wa Jimbo la Arumeru la Mashariki ameishukuru Serikali kwa kuongeza thamani ya Jimbo la Arumeru Mashariki kwa ujenzi wa shule hiyo.

Aidha, katika utatuzi wa changamoto za upatikanaji wa maji, kuongeza miundombinu ya taka, Nyumba za Walimu na Genereta zilizowasilishwa na Mwl.Janeth Mollel ambaye ni  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Patandi Maalum, Mhe. Silinde  ameeleza kuwa Serikali imelipokea na itatoa fedha mapema .

Katika ziara hiyo Mhe.Waziri alikagua pia ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya Sekondari Sing'isi vilivyojengwa kupitia Programu ya EP4R.

Mhe.David Silinde(Mb)akizungumza  katika viwanja vya Shule ya Sekondari Patandi maalum.

Mhe.Dkt.John D. Pallangyo,  Mbunge wa Jimbo la Arumeru la Mashariki

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo (kulia)akizungumza wakati wa ziara ya Mhe. Silinde.



Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa