Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt.Festo Dugange (MB) ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Wilayani Arumeru kwa kukusanya mapato kwa asilimia 107% kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na kupeleka asilimia 46% ya mapato hayo kwenye miradi ya Maendeleo.
Dkt.Dugange ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Wakuu wa Divisheni/Vitengo na Watumishi wengine wa Halmashauri hiyo? ambapo amepongeza pia ukusanyaji mapato kwa Mwaka huu wa fedha 2022/2023 kwani Halmashauri hiyo imekusanya mapoto kwa asilimia 58% kufikia mwezi Desemba 2023 na asilimia 74 % kufikia Machi 2023,ambapo ametoa Wito kwa Uongozi wa Halmashauri kuweka mikakati ya kuhakikisha Miradi yote inayopelekewa fedha na Serikali au mapato ya ndani inakamilika kwa wakati ili kuwa na tija zaidi.
Dkt.Dugange amehimiza Halmashauri kuhakikisha zinaongeza ufanisi kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuongeza wigo wa kujitegemea .Pia kuhakikisha katika fedha zinazokusanywa zinatengwa fedha kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo " Kusanyeni mapato kwa ufanisi Mkubwa, tekelezeni miradi kwa tija .Pia toeni fedha za mikopo isio kwa tija zaidi" amehimiza Dkt.Dugange
Aidha kikao Hicho cha Mhe.Naibu Waziri wa TAMISEMI kimewajumuisha viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.John D Pallangyo,Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Wilaya,Viongozi ngazi ya Mkoa. Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Arumeru,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe
Jeremia Kishili na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa