• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

NDG,JOHN D. PALLANGYO APITA BILA KUPINGWA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI.

Imewekwa: April 19th, 2019

Mgombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi, (C.C.M) Ndg.John Pallango atangazwa rasmi  kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, msimamizi wa uchaguzi  mdogo  jimbo la Arumeru Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Meru Ndg. Emmanuel Mkongo amemtangaza John D. Pallangyo  kupita bila kupingwa kwenye Uchaguzi mdogo wa Ubunge jimboni humo.

Mkongo amesema kuwa  toka  zoezi la kuchukua fomu lianze tarehe April 15 Aprili mwaka 2019, jumla ya  wagombea 11 walijitokeza kuchukua fomu lakini hadi kufikia 10:00 jioni ya leo wagombea watatu ambao ni Antonia Ndosi (DP),George Nashoni (CUF) Msifuni Mwaja (TL)  walishindwa kurudishwa fomu.

Aidha Mkongo ameeleza kuwa wagombea wengine saba ambao ni Mohamed Kitundu (SAU),Juma Ntajera  (ADA- TADEA), Tulisabya Lwitakubi (UNDP),Mgina Mustafa (AAFP) Rashid Mkama (NRA),Cosmas Kavishe(NCCR) Mageuzi, Saimon Ngilisho(Demokrasia Makini) wa vyama vya upinzani walirejesha fomu lakini wakati wa ukaguzi  NEC ilibaini fomu zao kuwa na dosari mbalimbali zilizosababisha kuenguliwa kwenye mchakato huo.

 Akizungumza mara baada ya kutangazwa kupita bila kupingwa Ndg.John Pallangyo ameishukuru NEC kwa kufanya kazi yake kwa uadilifu pamoja na mwenyekiti wa CCM taifa Rais John Magufuli kwa kupitisha jina lake kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM ili apeperushe bendera ya CCM.

Aidha Pallangyo amewahidi wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki  kuwa atashirikiana nao kutatua kero walizo nazo mara baada ya kuapishwa.

Aidha wagombea saba ambao hawakukidhi vigezo  vya NEC,wamekiri kuridhika na matokeo ya uteuzi  wa Ndg. John Pallangyo na kuahidi kumpa ushirikiano  wa kutosha. 

Naye mshili mkuu wa viongozi wa mila na tamaduni za  Meru Ezron Summary alimuomba Mbunge huyo mteule kushirikina na wananchi wa Meru na kuwaletea maendeleo.

Ikumbukwe kuwa zoezi la urejeshaji fomu za kugombea ubunge  Jimbo la Arumeru Mashariki  lilianza tarehe 15 Aprili 2019 na kuhitimishwa leo Tarehe 19 Aprili 2019 saa 10:00 kamili jioni.


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa