Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Meru Daniel Mwakitalu amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata, Vijiji na Waandikishaji wa daftari la wapiga Kura kufuata kanuni na miongozo iliyowekwa kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Mwakitalu ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya mafunzo Kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata, Vijiji na Waandikishaji wa daftari la wapiga Kura yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Msingi silver leaf Academy Usa-River. Aidha katika Hafla hiyo Mwakitalu amemuawakilisha msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya.
Aidha Katika Hafla hiyo waandikishaji wa daftari la wapiga Kura wamekula kiapo cha utii wa utekelezaji wa Jambo hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa