Wananchi wa Kata ya Ngabobo, Halmashauri ya Wilaya ya Meru waiomba Serikali kusajili Shule ya Msingi Oltepesi Ili wanafunzi wapate Elimu katika umbali mdogo.
Wananchi hao wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ya kukagua na kutembelea ujenzi wa vyumba Vitatu vya Madarasa, matundu ya vyoo na nyumba ya mwalimu itakayokaa familia mbili Shuleni hapo.
Aidha Mwl.Makwinya amepongeza jitihada za Wananchi na Viongozi kuhamasisha shughuliza za maendeleo ambapo ameielekeza Idara ya Elimu Msingi kuwashauri na Kuwasaidia Wananchi hao Ili Shule hiyo iweze kusajiliwa.
Vilevile Kata ya Ngabobo inatekeleza Ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambapo walipokea fedha kutoka serikali kuu, Diwani wa Kata ya hiyo Mhe.Lenyumbu Kinua ameishukuru Serikali kutoa Milioni 50 kwaajili ya ujenzi wa Jengo la mama na mtoto pamoja na Nyumba ya Mtumishi itakayokaa familia mbili.
Aidha Mhe.Kinua ameiomba Halmashauri Kusaidi baadhi ya miundombinu ikiwemo kichomea taka na shimo la kuhifadhi Kondo la nyuma.
Kata ya Ngabobo ni Miongoni mwa Kata saba ambazo Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya (nguo rangi nyekundu) akikagua ujenzi wa vyumba Vitatu vya Madarasa katika Shule tarajali ya Msingi Oltepesi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya (nguo rangi nyekundu) akikagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu (two in one) katika Zahanati ya Ngabobo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya (nguo rangi nyekundu) akikagua ujenzi wa Nyumba ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Ngabobo.
Jengo la mama na Mtoto katika Zahanati ya Ngabobo .
Diwani wa Kata ya Ngabobo Mhe.Lenyumbu Kinua (wa Kwanza kulia)wakati wa Ziara ya Mkurugenzi katika Kata ya Ngabobo.
vyumba Vitatu vya Madarasa katika Shule tarajali ya Msingi Oltepesi
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa