Wahasibu wa Shule za Sekondari na Msingi kwenye Halmashauri ya Meru,Wakuu wa Shule na Walimu wakuu wapewa semina elekezi juu ya matumizi ya Mfumo mpya wa Facillity Financial Accounting and Reporting System(FFARS) ,
Mtoa maada mkuu kwenye mafunzo hayo ya FFARS, Emmanuel Joramu ambaye ni mweka Hazina wa Halmashauri hiyo amesema mfumo huo wa uhasibu na utoaji taarifa (FFARS) utawezesha ufuatiliaji wa matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali na taarifa zake zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma kwenye vituo vya kutolea huduma vikiwemo shule,vituo vya afya na hospitali za wilaya Pia utaongeza uwazi, na hivyo kuwezesha jamii kupata huduma bora.
Nao Wahasibu waliohudhuria mafunzo hayo ya FFARS yaliyofanyikia katika ukumbi wa Shule Msingi Amani wamesema Mfumo huo utawarahisishia uandaaji ,upataji na utoaji wa taarifa za fedha.
Eliringia A. Uisso ambaye ni mkuu wa shule ya Songoro Ameeleza kua mfumo huu utarahisisha uandaaji wa bajeti za shule pamoja na kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kuzingatia bajeti hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa