Benki ya NMB yakabidhi vifaa tiba kwa zahanati ya Kikatiti ikiwa ni kuunga mkono mwamko wa ukamilishaji wa zahanati hiyo uliofanywa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambapo alichangia milioni 10 za ukamilishaji wa zahanati hiyo wakati akisalimiana na wananchi wa Kikatiti Oktoba 2021.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba hivyo Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Bwn.Dismas Prosper amesema benki hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuwaletea wananchi maendeleo ambapo imetoa kitanda cha kujifungulia kinamama ,kitanda cha wagonjwa godoro, mzani wa kuwapima uzito wagonjwa, mizani mbili ya kupimia wtoto wanapozaliwa ,stendi za dripu katika zahanti ya kikatiti na katika sekta ya elimu benki hiyo imetoa bati 130 kwa shule ya Sekondari Umoja King'ori hivyo jumla ya michango hiyo ni Shilingi Milioni saba.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ameipongeza Benki ya NMB kuunga mkono juhudi za Serikali za uboreshaji wa huduma za afya sambamba na miundombinu katika sekta ya elimu ambapo ameendelea kuikaribisha Benki hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali kuwaletea maendeleo wananchi "leo tumeshuhudia wananchi hawa wa Kikatiti wakituma salamu za shukrani kwa Mhe .Rai , tunaipongeza NMB kuunga mkono hamasa hii ya Mhe.Rais"amesema mhe Ruyango
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameishukuri Benki ya NMB ikiwa ni mdau wa pili kuunga mkono ukamilishaji wa zahanati ya Kikatiti baada ya Shirila la Cross Talent Share International (CTSI) kuchangia milioni 135.38 hadi sasa katika ukamilishaji wa zahanati hiyo.
Makwinya amesema baada ya Mhe.Rais kuchangia Milioni kumi za ukamilishaji wa zahanati ya kikatiti, hamasa ilianza na Halmashauri ilichangia milioni 10 na Mbunge kupitia mfuko wa jimbo alichangia Milioni 5 ambapo mwamko huo umeendelea kwa wadu wa CTSI na NMB.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili ameishukuru benki ya NMB kuitikia hamasa ya ukamilishaji wa zahanati ya Kikatiti aliofanya Mhe.Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" Zahanati hii ilisimama takribani miaka tisa ikiwa boma, lakini Mhe. Rais alipoweka mkono wake hamasa imekua kubwa na wananchi watanufaika na huduma " ameeleza Mhe.Kishili
Wananchi wa Kijiji cha Kikatiti wamemshukuru Mhe. Rais kuamsha ukamilishaji wa zahanati yao kwani kupitia mchango wake Halmashauri na Wadau wamechangia, pia Serekali imeleta wataalumu watatu katika zahanati hiyo "Tunamshukuru Mhe. Rais, tunaishukuru NMB kwani vifaa hivi vitatumika katika utoaji wa huduma na kutuondolea kero kubwa na gharama za kupata huduma za afya katika umbali mrefu" amesema Mwenyekiti wa Kijiji cha Kikatiti
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza katika hafla ya NMB kukabidhi vifaa tiba.
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini Bwn.Dismas Prosper akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba.
Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa