Benki ya NMB kupitia Tawi la Usariver ambao ndio wenyeji wa kongamano Maalum la walimu linalojulikana kama "Mwalimu Spesho" wameandaa kongamano la kutoa elimu kwa Walimu kuhusu masuluhisho mbalimbali ya kifedha.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Godson Majola Halmashauri ya Wilaya ya Meru huku Mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya.
Kongamano hilo lenye lengo la kujadili fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB kwa walimu lakini pia, kupokea mrejesho wa huduma zinazotolewa kwa walimu ili kuweza kuboresha huduma hizo.
Mgeni rasmi, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ameeleza kuwa kongamano hilo litawasaidia walimu kujua fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB lakini kuwajibika katika kazi kwani walimu wanapokea Fedha za ruzuku na fedha za maendeleo katika maeneo yao.
" Mafunzo yanayotolewa katika kongamano hili yatawasaida walimu kupata elimu ya namna bora ya matumizi na udhibiti wa fedha za Serikali" Ameeleza Makwinya.
Aidha, Meneja wa Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus ameeleza kuwa walimu ndio kundi kubwa la wateja wanaopatiwa huduma kupitia benki ya NMB na kupitia walimu benki ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake.
Hata hivyo, Meneja Mwandamizi Huduma binafsi kutoka Makao Makuu Bi. Queen Dickson ameeleza kuwa, kongamano hilo la walimu wamelenga kutoa elimu kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB kama vile kutoa Elimu ya Fedha, Mikopo, Bima, na usalama wa Fedha kupitia mfumo wa wa ESS " Employee Self Service" pamoja na kutoa elimu ya aina ya mikopo inayotolewa na benki ya NMB kama vile Mikopo ya Elimu,NMB faraja, Mikopo Maalum ya Biashara, Mkopo wa nyumba, Mkopo wa Bima, Mkopo wa Kilimo cha Mkataba, kufungua Akaunti ya akiba ya Ada ya Mtoto na Mikopo mingine inayotolewa na benki hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Lakitatu Mwl. Nompi Marcel Ngoly ametoa shukrani kwa NMB kwa kutoa elimu katika kongamano hilo kwani itawasaidia kujua fursa mbalimbali lakini pia kuwasaidia walimu wengine ambao hawakupata nafasi ya kushiriki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa