Mkuu wa Idara ya Serikali Benki ya NMB Vicky Bushubo (alievaa miwani kwenye Picha ya Kwanza) ametoa shukrani Kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya Kwa Ushirikiano anaouonyesha Kwa Benki hiyo.
Bushubo ametoa shukran hizo wakati alipofika Ofisi ya Mkurugenzi Kwa Ziara fupi ya kikazi yenye Lengo la kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa na NMB katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru hasa katika utoaji Huduma Kwa watumishi. Aidha katika Ziara hiyo aliambatana na viongozi mbali mbali wa Benki ya NMB akiwemo meneja mahusiano mwandamizi kutoka makao makuu, meneja mahusiano kanda ya Kaskazini na meneja wa NMB Kata ya Usa-River.
"Nikiwa kama muwakulishi wa NMB kutoka makao makuu tunatoa shukran za dhati Kwa Ushirikiano unaotupatia kwani tunapata mrejesho wa jinsi unavyoshirikiana na Watendaji wetu katika Halmashauri yako na hatujapata Taarifa yoyote ya changamoto baina ya Ofisi yako na Ofisi zetu hivyo ni dhahiri kuwa kazi inakwenda vyema nipende kutoa shukrani hizi" Bushubo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya pia ametoa shukran za dhati na Kwa Ushirikiano unaonyeshwa na Benki ya NMB na kusema kuwa ushirikiano anaouonyesha ni Moja ya majukumu yake kwani anapaswa kutoa ushirikiano Kwa Taasisi zote za Serikali na zisizo za kiserikali ili Kujenga mahusiano Bora ya kiutendaji.
NMB mara baada ya kikao hicho kifupi imempatia zawadi Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Makwinya kama ishara ya ushirikiano mwema.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa