Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili amewapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuzalisha watu mashuhuri katika Taifa hili.
Mhe. Kishili amesema " nyie ni watu wa muhimu kwani ndio mnaozalisha watu mashuhuri katika Taifa hili mfano mwalimu anazalishwa na mwalimu, Daktari anazalishwa na mwalimu, Rubani na fani yoyote katika Dunia hii inazalishwa na mwalimu hivyo tunawapongeza kwa kazi hii kubwa yakitume mnayoifanya Mungu awabariki sana"
Mhe. Kishili amezungumza hayo kwenye tamasha la kuwapa pongezi na kutoa motisha kwa walimu Meru DC lililofanyika katika Chuo Cha Ualimu Elimu maalumu Patandi leo tarehe 25 Julai 2024
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa