Na Annamaria Makweba
Maafisa Ugani wa Mifugo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wamekabidhiwa pikipiki sita kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za ugani katika Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Akikabidhi Pikipiki hizo zenye namba za usajili STM 6349, STM 6350,STM 6351,STM 6352,STM 6353,STM 6354, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Kaganda amewataka Maafisa Ugani kuhakikisha pikipiki hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
" Pikipiki hizi ni mali ya Serikali na hairuhisiwi kuzifanyia biashara ya Bodaboda, zitumike kwa kazi kwa ajili ya kusaidia jamii katika kutoa huduma za masuala ya ugani" Alisema Kaganda.
Hata hivyo, Kaganda ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha Sekta mbalimbali na kuhakikisha Vitendea kazi vinapatikana ili watumishi kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa