Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) Kanda ya Kaskazini wamekutana na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa lengo la kujitambulisha na kueleza masuala mbalimbali yanayohusu Ununuzi wa Umma.
Kikao hicho kimefanyika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambapo wamepokelewa na Afisa Utumishi Mkuu Furahisha Magubila pamoja na Menejimenti ya Halmashauri hiyo.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini Magai Malekela Maregesi amesema kuwa Serikali imeanzisha ofisi za kanda katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kanda ya Kaskazini, Njanda za juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini na Kanda ya Pwani ili kusogeza huduma karibu kwa taasisi za serikali na umma kwa ujumla
Aidha, Maregesi ameeleza kuwa Serikali imejenga mfumo wa Ununuzi wa Kieletroniki ( NeST) ili kuweka uwazi, uwajibikaji, kupunguza mianya ya rushwa, kuondoa upendeleo na kuwa na usalama wa taarifa ili serikali iweze kupata thamani ya fedha na kufanya shughuli za ununuzi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Hata hivyo, Maregesi ameeleza kuwa miongoni mwa majukumu ya PPRA ni pamoja na kuishauri Serikali kuhusu masuala yote ya ununuzi. Lakini, pia kufanya ukaguzi na uchunguzi katika masuala ya manunuzi pamoja na kuwajengea uwezo taasisi nunuzi na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kushiriki kwenye manunuzi ya umma.
Vilevile, amesisitiza Halmashauri kuhakikisha inafuata taratibu zote za manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa miradi kwa kutumia mfumo wa NeST katika shughuli zote za utekelezaji wa miradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa