Tarehe 23 Septemba 2019 Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jonathan Kiama alitoa maelezo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, Mwaka 2019 katika Mkutano wa hadhara ya wadau wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa Vyama vya Siasa.
Kiama alieleza kuwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika tarehe 24 Novemba 2019 na Uandikishaji utaanza tarehe 08 hadi 14 Octoba 2019 katika Vitongoji 330 na Vijiji 90 vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo kutakua na Vituo 330 vya kuandikisha wapig a kura vitavyo funguliwa kuazia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Aidha.Uchaguzi utafanyika tarehe 24 Novemba 2019,katika vitongoji 330 na vijiji 90 vya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo kutakuwa na Vituo 330 vya kupiga kura vitakavyo funguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Kiama aliwasisitiza wakazi wote wa Halmashauri ya Meru , wenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa. Tarehe 24 Novemba 2019 pia ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri hiyo wenye Umri wa Miaka 21 au Zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Kitongoji, uenyekiti wa Kijiji na ujumbe wa Halmashauri ya Kijiji kuchukua fomu za kugombea zitakazo patikana kwenye ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
Fomu za maombi ya kugombea uenyekiti wa Kijiji, uenyekiti wa Kitongoji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji zitachukuliwa tarehe 29 Octoba 2019 saa 1:30 asubuhi na kurejeshwa tarehe 04 Novemba 2019 ambapo mwisho wa kupokea fomu ni saa 10:00 kamili jioni.Fomu hizo zitatolewa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi. Siku ya uteuzi wa wagombea ni tarehe 5 Novemba 2019, fomu za wagombea zitabandikwa kwenye mbao za matangazo.
Aidha, Uwasilishaji wa Pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea yeyote ni kuanzia tarehe 05 hadi 06 Novemba 2019 na uamuzi wa pingamizi kuhusu uteuzi wa mgombea ni tarehe 05 hadi 07 Novemba 2019 na Rufaa dhidi ya uamuzi wa Msimamizi msaidizi wa uchaguzi ni tarehe 05 hadi 08 Novemba 2019.
Mikutano ya Kampeni itafanyika kwa siku 7 kuanzia tarehe 17 hadi 23 Novemba 2019 ambapo itaanza saa 2:00 asubuhi na kumalizika saa 12:00 jioni ya kila siku ya Kampeni.
Kiama amehitimisha kwa kutoa wito Wananchi wa Halmashauri ya Meru kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa amani kulingani na kanuni ya 35(6)mtu yeyote hataruhusiwa kubaki eneo la kupiga kura baada ya kupiga kura.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa