Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda amekagua mradi Wa shilingi Milioni 900 wa Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Meru na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea katika hospitali hiyo.
Akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa mradi huo, Eng. Asnathi Marero ameeleza kuwa mradi huo ambao kwa sasa umetumia shilingi zaidi ya Milioni 399 umeweza kujenga Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, jengo la famasi na Kichomea taka cha kisasa ambayo yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Rc Makonda ameeleza kuwa mbali na utekelezaji huo kuendelea vizuri, ametoa maelekezo ya kuongeza kasi na kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya miezi miwili ili mradi huo uweze kuwa na tija kwa wananchi na kuweza kupata huduma katika hospitali hiyo.
Aidha, wananchi wametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha na kujenga miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Meru na kwa mradi huu baada ya kukamilika utaboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa