Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameelekeza Halmashauri ya Meru kwa ushirikiano wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri kubuni mpango wa kuwezesha kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wanaopatikana katika Wilaya ya Arumeru.
RC Makonda , ametoa maelekezo hayo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alipokuwa akizungumza na Watendaji wa Wilaya hiyo kabla ya kuendelea na ziara yake inayoendelea katika Wilaya hiyo Mkoani Arusha.
Akizungumza na viongozi mbalimbali, RC Makonda ameeleza kuwa Halmashauri ya Meru ina Ardhi nzuri na yenye rutuba inayoweza kuwasaidia wananchi kuondokana na hali ya umasikini na kukuza uchumi.
" Tuweke ajenda zetu za kuanzisha eneo maalum la mazao na kuchakata wenyewe na kusafirisha nje ya Nchi na siyo watu wa nje kuchukua mazao yetu kuchakata na kuweka nembo yao na kupata fedha nyingi wakati hili lipo ndani ya uwezo wetu. Amesema Makonda.
Aidha, RC Makonda amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Mkurugenzi Mtendaji kukemea watumishi ambao hawafanyi kazi za kuwaletea wananchi Maendeleo na badala yake kujipendekeza kwa viongozi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa