Taasisi ya Saidia Tanzania Community Foundation (SATACOFO) yatoa msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanafunzi waliopo katika shule za Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mfadhili wa Taasisi hiyo Bw. Damien Sellier amekabidhi vifaa hivyo Leo ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na Jezi za kuchezea pamoja na mipira.
Katika makabidhiano hayo Bw. Damien amesema kuwa wanajishughulisha katika kuwezesha shughuli mbalimbali za maendeleo na kusaidia masuala ya Elimu na Michezo.
Aidha, Katibu wa Taasisi hiyo Bw. Raymond Julius amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kutoa ushirikiano mkubwa pamoja na maafisa wa Halmashauri kwa kupitia Afisa michezo wa Halmashauri Bw. Daniel Nanyaro.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa