Watumishi wapya 16 waliofuzu usaili wa nafasi ya Mtendaji wa Kijiji,Katibu Mhutasi,Dereva na Msaidizi wa Hesabu, uliofanywa na Halmashauri ya Meru Tarehe 09 -10 Octoba 2017 wafundishwa maadili ya utumishi wa Umma pamoja na kupata elimu ya kina juu ya kutekelezamajukumu yao kwa ufanisi pamoja na kujaza Fomu za Mkataba wa Ajira Serikalini pia kukamilisha ujazaji wa fomu na taarifa zote zilizokua zinahitaji.
Aidha Semina hii imefanywa na Halmashauri ya Meru kupitia idara ya Utumishi na Rasilimali watu ikiwa ni baada ya vyeti vya watumishi hawa kuhakikiwa na Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) na kuthibitika kua ni halali.
Akizungumza na watumishi mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Grace A. Mbilinyi amewasisitiza watumishi hao kutumia mafunzo haya yatakayo wawezesha kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ,Kanuni Na Taratibu za Utumishi wa Umma.
Aidha Semina hii elekezi kwa watumishi wapya imefanyika kwa siku mbili Tarehe 28-29 Novemba kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa