Semina ya uelewa juu ya uendeshaji wa Mabaraza ya Kata ambayo kwa mujibu wa sheria yana nguvu mbili kisheria ambayo ni nguvu shurutishi na nguvu suluhishi imefanyika leo katika ofisi ya kata ya Maruvango washiriki wakiwa ni wajumbe wa mabaraza ya kata toka kata ya Leguruki na Maruvango.
Semina hii imeandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupitia kitengo cha Sheria na kuwasilishwa katika kata hizi na mwanasheria Prosper Ndomba ambaye amesema zoezi hili la utoaji semina kwa Mabaraza ya Kata linaendelea kufanyika kwa kata zote ,Wajumbe wamekiri kupata uelewa mkubwa juu ya uendeshaji wa Mabaraza hayo wenye lengo la kupunguza migogoro isiyo ya lazima.
Mjumbe Zakaria I. Akyoo alitoa angalizo kwa kuhoji ``Halmashauri ina mpango gani kuhakikisha chombo hichi kilichoundwa kwa mujibu wa sheria hakidhaliliki kwa kukosa hata chumba cha ofisi" tena kujibiwa kwa kufafanuliwa kuwa Afisa mtendaji wa kata ndiye mratibu wa Mabaraza hayo kwa ngazi ya kata husika hivyo ataratibu maswala kama hayo.
Naye Mheshimiwa Diwani wa kata ya Maruvango Samwel I. Nnko amewasihi wajumbe wa Mabaraza hayo ya kata kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kutozingatia mengine kama vile undugu,Diwani huyo amewashauri wajumbe hao kutii mamlaka za juu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa