Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka historia katika Sekta ya Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo ilitoa Shilingi Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Amsha katika kata ya Ambureni ambayo haijawahi kuwa na Shule ya Sekondari kwa miaka 14 toka Halmashauri ya Meru kuanzishwa Mwaka 2007.
Mwaka 2022 Serikali ya awamu ya sita imeweka historia kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kupangwa wote kwa awamu moja bila kusubiri awamu nyingine hii ni kutokana na uwepo wa madarasa na samani za kutosha ambapo Serikali ya awamu ya sita ilitoa Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya 70 vya madarasa na samani zake (Meza na Viti) katika shule za Sekondari 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Meru .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa